Wednesday, October 16, 2013

mauaji Chunya,huku wahabeshi wawili wakishikiliwa na mtu anayedaiwa dalali wa biashara haramu ya binadamu mkazi wa kasumulu akitiwa mbarano




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 16. 10. 2013.


WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NKUHUNG’U KATA YA LUPA, TARAFA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.  MATHA D/O CHARLES,  MIAKA 32,  MFIPA, MKULIMA, MKAZI WA NKUHUNG’U,  ALIFARIKI DUNIA AKIWA NYUMBANI KWAKE BAADA YA  KUPIGWA KWA FIMBO MGONGONI NA MBAVUNI NA MUME WAKE AITWAE JOSEPH S/O JOHN, MIAKA 40, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA NKUHUNG’U SIKU YA  TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA  SAA 02:45HRS . CHANZO NI UGOMVI WA KIFAMILIA. BAADA YA  TUKIO MTUHUMIWA ALIMKATAZA MAREHEMU KWENDA HOSPITALI KUPATA MATIBABU HIVYO KUUGULIA NYUMBANI HADI ALIPOFARIKI DUNIA.  MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII HASA WANAFAMILIA/NDOA KUTATUA MATATIZO YAO KWA KUJENGA HOJA NA  KUKAA MEZA MOJA YA  MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA KYELA – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE 15.10.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO KASUMULU WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. ZALAKA S/O KABHAM, MIAKA 20 NA 2. ERISIDO S/O KAPARA, MIAKA 25, WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO NA KUHIFADHIWA NA DENIS S/O ANORD, MIAKA 20, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA KASUMULU AMBAYE PIA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA  MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE MARA MOJA.






Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Tuesday, October 15, 2013

mauaji ya kutisha Mbeya,Mbarali nako gari lauwa na kujeruhi




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15. 10. 2013.



WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – MAUAJI.

MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO KATIKA MSITU WA IHONDO KIJIJI CHA MALANGALI KATA YA SWAYA MPAKANI MWA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI NA WILAYA YA   RUNGWE MKOA WA MBEYA. MICHAEL S/O WILLIAD, MIAKA 24, MSAFWA, M/BIASHARA, MKAZI WA MALANGALI WILAYA YA  RUNGWE, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA KICHWANI NA MWILI WAKE KUTUPWA KATIKA MSITU WA IHONDO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA ANATOKA MBEYA MJINI KUNUNUA MAHITAJI/BIDHAA NDOGO NDOGO ZA DUKANI KWAKE AKIWA NA PIKIPIKI YAKE  T.819 CDQ AINA YA  T-BETTER NA KUMUUA KISHA KUMTUPA MSITUNI. PIKIPIKI YA MAREHEMU ILIKUTWA NJIANI IMEEGESHWA IKIWA NA BIDHAA ALIZOKUWA AMENUNUA. CHANZO KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
                                                  KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI
.

MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 07:15HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA META - IGURUSI BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.404 AAT AINA YA TOYOTA MARK II LIKIENDESHWA NA DEREVA SAAD S/O MWATOVENE, MIAKA 71, MSANGA, MKAZI WA CHIMALA LILIMGONGA MPANDA BAISKELI REHEMA D/O KUNDAMA, MIAKA 21, MHEHE, MKULIMA, MKAZI WA MAPUNGA – IGURUSI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE DANIEL S/O GEORGE, MIAKA 21, MUWANJI, MKULIMA, MKAZI WA IGURUSI AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA CHIMALA- MISHENI NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.









WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI  WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA RAMADHAN S/O JUMA, MIAKA 31, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MAKONGOLOSI AKIWA NA BHANGI DEBE MOJA SAWA NA UZITO WA KILO 10. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.


WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [RIFFLE].

MNAMO TAREHE 13.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA LUKWATI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI  WAKIWA DORIA/MSAKO  KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA HIFADHI HIYO WALIMKAMATA SAMOLA S/O DAMAS, MIAKA 41, MBUNGU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA GUA AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA  RIFFLE NA RISASI MBILI [02]. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZILIZOWEKWA. 

WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – KUFA MAJI.

MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO MTO MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. MTOTO AITWAYE YUSUPH S/O TIMOTH, MIAKA 12, KYUSA, MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO [05] SHULE YA MSINGI IWINDI ALIFARIKI DUNIA KATIKA MTO HUO WAKATI ANAOGELEA. UCHUNGUZI WA AWALI UMEBAINI KUWA MAREHEMU ALIKUWA AKISUMBULIWA NA TATIZO LA KIFAFA HALI ILIYOSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIOGELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA WILAYA – IFISI.  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO ILI KUWEZA KUEPUKA MADHARA/MATATIZO YANAWEZA KUWAPATA WATOTO WAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI WAISHIO MAENEO YENYE VYANZO VYA MAJI KUCHUKUA TAHADHALI KWA WATOTO WAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.



                                                                Signed by:

[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Monday, October 14, 2013

MKE NA MUME WATEKETEA KWA MOTO MBEYA MJINI,NOTI BANDIA ZAKAMATWA MBOZI




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 14. 10. 2013.

WILAYA YA  MBEYA MJINI – AJALI YA  MOTO NA KUSABABISHA VIFO.

MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA  SAA 00:25HRS HUKO ILEMI JIJI NA MKOA WA MBEYA. FADHIR S/O SAID, MIAKA 45, MMAKUA, MKAZI WA ILEMI NA  MKE WAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUCY D/O SAID,  MKAZI WA ILEMI, WALIRAFIKI DUNIA  KWA KUUNGUA MOTO WAKIWA KATIKA MOJAWAPO YA VYUMBA VYA NYUMBA YAO.  CHANZO CHA MOTO HUO BADO KUFAHAMIKA. NYUMBA HIYO ILIYOKUWA INAMILIKIWA NA MAREHEMU HAO  INA JUMLA YA  VYUMBA SITA [06] NA SEBULE MOJA  NA MAREHEMU ALIKUWA ANAISHI NA FAMILIA YAKE YENYE WATOTO WANNE. MOTO ULIZIMWA NA WANANCHI  WA ENEO HILO KWA KUSHIRIKIANA NA  POLISI WALIOFIKA ENEO HILO. HAKUNA MADHARA KWA WATU WENGINE. YALIYORIPOTIWA KUTOKEA, THAMANI HALISI YA  MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. MIILI YA  MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI YA  KUJIEPUSHA NA MAJANGA YA  MOTO.

WILAYA YA  MBOZI – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.

MNAMO TAREHE 13.10.2013 MAJIRA YA  SAA 18:00HRS HUKO MLOWO WILAYA YA  MBOZI MKOA WA MBEYA.  ERICK S/O KYANDO,MIAKA 32,  MKINGA, FUNDI MAGARI, MKAZI WA ILEMBO MLOWO – MBOZI  ALIKAMATWA NA NOTI BANDIA ZA KITANZANIA TSHS 100,000/= [ZOTE ZIKIWA NOTI MPYA ZA TSHS 10,000/=] AMBAZO ALITAKA KUINGIZA KWENYE AKAUNTI YAKE YA  M-PESA KWA WAKALA AITWAE LYIDIA D/O MWAKIPESILE. NOTI HIZO ZINA NAMBA – BF 29378331 NOTI -3, FC- 4243042 NOTI -1, FC- 4243043 NOTI -2, AA-4243031 – NOTI 1, BF- 4243045 NOTI 2 NA AA 4243034 NOTI 1. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUWA NA TAHADHARI NA MATUMIZI YA  PESA HASA NOTI ILI KUEPUKANA NA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU AU MTANDAO UNAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI/USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

WILAYA YA  MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 13.10.2013 MAJIRA YA  SAA 13:30HRS HUKO KATIKA KITUO  KIDOGO CHA POLIS  UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI  WALIMKAMATA SAIMON S/O KISUNGU, MIAKA 22, MUWANJI, MKULIMA, MKAZI WA SIMAMBWE AKIWA NA BHANGI KETE MOJA MFUKONI SAWA NA UZITO WA GRAM 5,  WAKATI AKIPEKULIWA BAADA YA  KUKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI. TARATIBU ZINAFANYWA  ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

                                                       Signed by:

[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.